Alhamisi 26 Juni 2025 - 19:40
Ushindi wa kujivunia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kielelezo cha heshima kwa Umma wa Kiislamu mbele ya ubeberu wa kimataifa

Hawza/ Hujjat-ul-Islām wal-Muslimīn Sayyid Hassan Mousavi, katika ujumbe wake, ameeleza kwamba: ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni ni dhihirisho la heshima, uthabiti na mwamko wa Umma wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjat-ul-Islām wal-Muslimīn Sayyid Hassan Mousavi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kisheria ya Mashia wa Jammu na Kashmir, katika ujumbe wake, ameupongeza ushindi wa kujivunia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na uvamizi wa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake wa kimataifa, hususan Marekani, na akautaja kuwa ni ishara wazi ya uwezo, busara na imani ya taifa la Iran.

Amesema katika ujumbe huo: “Ushindi huu mkubwa naupongeza kwa dhati kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mheshimiwa Ayatollah al-‘Uz‌mā Sayyid Ali Husseini Khamenei (Mwenyezi Mungu adumishe kivuli chake kitukufu juu yetu), vikosi vya jeshi vilivyo na fahari, na taifa lenye subira na uelewa la Iran. Mafanikio haya si tu matokeo ya kijeshi, bali ni dhihirisho la wazi la imani, hamasa, jitihada za kutafuta heshima, na kustahimili dhidi ya watawala wa dunia.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kisheria ya Mashia wa Jammu na Kashmir, akizungumza kuhusiana na nafasi maalumu ya Iran katika kuwatetea watu wanaodhulumiwa duniani, ameongeza kuwa: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikulinda tu mipaka yake, bali pia imekuwa sauti ya wazi ya mataifa yaliyoko chini ya dhuluma, na kwa kusimama kidete kwa ujasiri mbele ya utawala unaouwa-watoto wa Kizayuni na Marekani, imeonyesha kielelezo cha kivitendo cha uhuru na heshima kwa Waislamu wote na wanyonge duniani. Ushindi huu, kwa kweli, ni ushindi wa Umma mzima wa Kiislamu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha